Burudani

Hawa ndio mastaa Bongo waliofunga ndoa mwaka 2017

Kabla hatujaumaliza mwaka huu Bongo5, inakuleta orodha ya mastaa kutoka Bongo waliouaga ukapela kwa mwaka huu 2017. List hii inawahusu wasanii wa muziki,waimbaji wa injili,watangazaji na watayarishaji wa muziki.

1. Madam Frola

Baada ya kuachana na mumewe Emannuel Mbasha, Frola ama Mrs Daudi kwa sasa alitangaza kuolewa upya mwaka huu mwezi wa nne. Na ndoa yake ilifungwa Mkoani mwanza na kijana aitwaye Daudi.

2. Defxtro

Prodyuza wa muziki Bongo, Henry Minja a.k.a Defxtro au DX ambaye anafanya kazi zake Jijini Arusha katika studio za Noizmekah alifunga ndoa na mpezi wake mwezi wa sita mwaka huu.

3. Professa Jay

Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Huale a.k.a Profesa Jay alifunga ndoa mwaka huu na mzazi mwezie mwezi wa saba tarehe nane.

4. Babuu wa Kitaa na Kenedy The Remedy

Wote ni watangaziji wa kituo cha Clouds Media Group harusi zao hazikuachana sana japo Babuu alifunga ya Kiislamu mwishoni mwa mwezi Julai ila Kenedy The Remedy alifunga ya Kikiristo Agosti tano.

5. Zamaradi Mketema

Ndoa yake ilikuwa moja ya ndoa iliyovusta hisia za watu kutokana na habari zilziokuwa zikisambaa mitandaoni kwa kukatisha mahusiano yake na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds, Ndugu Ruge Mtahaba. Ndoa hii ilifungwa mapema mwezi wa Kumi.

6. Dogo Janja na Uwoya

Ndoa yao ilifungwa mwishoni mwa mwezi wa Kumi na ni moja ya ndoa ilayoleta maswali mpaka sasa kuwa je kweli ni ndoa, na kama ni kweli kwa nini mama mzazi wa Dogo janja na Uwoya hawakuonekana hata kwenye picha za sherehe hiyo?

7. Joti

Waliopata bahati ya kuitazma harusi hii kupitia YouTube Channel ya Bongo5 watakuwa wanajua kilichokuwa kikiendelea na kutokea ukumbini. Kiufupi tu ndoa hii ilifungwa kanisani na mrembo aitwaye Tumaini mwezi Agosti tarehe 28.

8. Rommy Jones

Huyu ni official Dj wa Diamon Platnumz, ndoa yake ilifungwa siku ya Jumamosi hivi mwezi wa kumi na mbili mwanzoni na iliudhuriwa na watu wake wa karibu akiwemo mzazi mwenzake na Diamond Platnumz, Zarina Hassan.

9. Shilole

Mrs. Uchebe, kulikuwa na minong’ono ya hapa na pale hatimaye kijana Uchebe ameweza kutimiza ahadi yake ya kumuoa bibie Zuwema maarufu kama Shilole mwezi huu wa kumi na mbili na harusui hii iliudhuliwa na watu wa karibu akiwemo Meneja wa Tip Top Connection Hamisi Tale ak.a Babu Tale.

10. Belle 9

Kutoka Moro Town , Abelinego Damian unaweza muita Belle 9 amefunga ndoa bhivi karibuniu na mpezni wake. Japo Belle mpaka sasa hajaongea choxchote ila kutoka kwa watu wake wa karubu wamempongeza kwa hatua hiyo muhimu katika maisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents