Habari

Hii ndio idadi ya vifaa vya NIDA vilivyoibiwa Arumeru, Jeshi la Polisi limeanza upelelezi

Hii ndio idadi ya vifaa vya NIDA vilivyoibiwa Arumeru, Jeshi la Polisi limeanza upelelezi

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linaendelea na upelelezi ili kuwabaini watu waliohusika na wizi wa vifaa vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), katika ofisi za NIDA zilizopo maeneo ya Arusha DC, wilayani Arumeru.

Vifaa vya NIDA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Polisi, wilayani Arumeru, Kamanda Mapunda, kupitia kwa Afisa Habari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Abel Stanford, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lililotokea usiku wa kuamkia leo Januari 6, 2020.

“Ni kweli kwamba kuna uvunjifu umefanyika maeneo ya Ofisi za NIDA hapo Arusha DC, wameiba Camera 2, Desktop 1, Laptop 2, ila Mratibu wa Polisi Arumeru yuko eneo la tukio anafuatilia, baadaye tutatoa taarifa kamili” amesema Abel.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents