Habari

Hiki ndio alichokizungumza Abdul Nondo baada ya kuachiwa huru hivi leo Iringa

Hiki ndio alichokizungumza Abdul Nondo baada ya kuachiwa huru hivi leo Iringa

Mahakama Kuu kanda ya Iringa, imemuachia huru aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Abdul Nondo, baada ya kukutwa hana hatia katika kesi ya Rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri, baada ya kutoridhishwa na hukumu yake aliyoshinda mwaka 2018.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Abdul Nondo.

Abdul Nondo ameachiwa leo Disemba 23, 2019, ambapo Mahakama imesisitiza kuwa hana hatia na kwamba hoja za rufaa za upande wa Serikali, zimeonekana kutokuwa na mashiko.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mara baada ya kushinda rufaa hiyo, Nondo amemshukuru Mungu pamoja na Mawakili wake waliosimama naye kuanzia mwanzo wa kesi hiyo, hadi leo alipoachiwa huru.

“Namshukuru Mungu sana,leo 23/12/2019 nimeshinda rufaa iliyofunguliwa na Jamhuri dhid ya maamuz ya kesi niliyoshinda Novemba 5, 2018, nawashukuru mawakili wangu Jebra Kanbole na Chance Luoga, Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC),pia Mahakama,ndugu na watanzania” ameandika Abdul Nondo.

Nondo alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutoa taarifa za uongo, kuwa alitekwa na watu wasiojulikana huku upande wa Jamhuri ukisema alijiteka mwenyewe.

Chanzo Eatv.tv.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents