Habari

Jangwani pamefungwa kisa Mafuriko – DART

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART umetoa taarifa kwa Watumiaji wa mabasi ya Mfumo wa DART kuwa leo Aprili 24, 2024, Barabara ya Jangwani imefungwa kutokana na mafuriko.

 

DART imesema Mabasi kwa njia za Kimara hadi Kivukoni na Gerezani yanaishia Magomeni Mapipa, pia huduma ya usafiri wa Mabasi ya DART inaendelea kutolewa kwa njia ya Morocco kwenda Kimara na eneo la katikati ya Jiji kwa njia ya Muhimbili na Gerezani.

“Huduma za Mabasi katika mfumo wa DART zinaendelea kama kawaida katika Njia Mlishi ya Kimara hadi Mbezi, Kimara hadi Kibaha na Kimara hadi Mloganzila”

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents