Habari

Je wajua kwanini watu hufukuzwa kazi?

Sio utani unaposikia kuna suala la kufukuzwa kazi kwani inakupunguzia ujasiri wako binafsi kwa familia yako, mke wako, watoto wako na hata jamii inayokuzunguka. Vile vile inaweza ikawa ni kitu cha kukufanya ujitambue zaidi na kujua kitu gani cha kufanya ingawa si rahisi, kwa urahisi ni kwamba kazi ilifikia mahali kwamba si ya kwako tena.

shutterstock_104307521

Wakati mwingine si kwasababu ya kiutendaji au ni mfanyakazi mwenyewe ana matatizo yake binafsi, hivyo inabidi afukuzwe kazi. Hebu fuatilia vitu vifuatavyo ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha wewe kufukuzwa Kazi;

1) Inawezekana haustahili kuwa sehemu hiyo:

Kumwajiri mfanyakazi kulingana na ujuzi wake ni muhimu sana kama yeye mwenyewe hastahili mahala hapo. Kama mtu hukustahili hapo na wakakuajiri kwa namna moja ama nyingine, madhara yake yataonekana tu. Madhara ambayo utakayaonyesha ni kushindwa kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

2) Kama wewe ni Mbishi na si msikivu:

Ukigundua kama wewe haustahili kwenye kampuni ulilopo, utangundua tu kwa vimbwanga na mambo yanayoendelea. Siku zote ukijiona una mzozo na wafanyakazi wenzako kila wakati, hauelewani na mabosi wako hiyo inaathiri utendaji wako wa kazi katika kampuni hiyo. Utagundua kila wakati kuna mgongano, hiyo  inakupunguzia ujasiri wako kiutendaji na vile vile unashindwa kufanya kazi sawasawa na inawezekana ukahisi kwamba watu wengine hawakupendi lakini kumbe wewe  mwenyewe una matatizo ya ndani, jichunguze halafu uone mabadiliko yatakuwaje?

3) Una tabia mbaya:

Tabia mbaya kwenye makampuni mengine ni sababu tosha ya wewe kuachishwa kazi. Wakati wote unapofanya kazi na watu wengine, haina maana sana kama wewe ni msengenyaji, mnafiki na mambo kama hayo. Wewe unakuwa mtengeneza sumu katika mazingira ya kazi. Si kwamba wale ambao hufikiri mabaya tu ni wabaya lakini kujua hayo mabaya wanayofikiri yanatoka kwa nani? na madhara yake yanaweza kusambaa kwenye kitengo kizima. Hivyo kupunguza uozo lazima ufanyike utaratibu wa kusafisha hali ya hewa.

4) Huwezi kuunganisha matukio:

Inawezekana katika majukumu na miradi mbalimbali huwezi kuleta vitu vyenye maana, huwezi kupangilia kazi na matokeo, huwezi kufuata muda na inawezekana kuna vitu vinaendelea kwenye maisha yako ambavyo vinasababisha ushindwe kufanya kazi kwa usahihi wake. kila jambo linapotokea unashindwa kuunganisha matukio au kupangilia mambo yako hivyo kuleta matatizo makubwa kwa bosi wako  na wafanyakazi wenzako. Kushindwa kwako kuona hayo madhaifu na kushindwa kujua matokeo ya baadaye kwenye mradi huo na hata kushindwa kuusimamia ipasavyo, unakuwa haufai kuendelea kuwepo hapo.

Hayo yote yanakufikisha huku kwenye;

5) Kutokuwa mtendaji wa kazi Mzuri:

Kushindwa kuunganisha mambo inasababisha wewe kuwa mzembe kwenye kazi zako za kila siku hivyo unakuwa unaiingizia hasara kampuni kwa kukulipa bila kufanya kazi ipasavyo. Wewe unakuwa ni mzigo kwa kampuni.

6) Wakati wote unakuwa mtu mwenye mawazo mengi au msongo wa mawazo:

Mtu kuwa na mawazo ni kawaida ila yanatakiwa yawe chini yako, vinginevyo hapo inakuwa ni mawazo ambayo yamekushinda hivyo inahatarisha utendaji wako na mahusiano yako na wafanyakazi wengine kazini. Kama unakuwa ni mtu mwenye mawazo na hauna furaha kwa muda mrefu inawezekana uko kwenye kazi isiyo sahihi na vile vile unaweza ukawa na msongo wa mawazo.

7) Unakuwa na matokeo ya kawaida kiutendaji:

Inawezekana unamaliza kazi na lakini utekelezaji wake ni wa kiwango cha kawaida au cha chini. Hivyo unakuwa hauwezi kuonyesha kitaaluma na kiutendaji wako kama una endana na elimu yako.

8) Unajikuta unaleta matatizo yako ofisini :

Hapa namaanisha mawazo na hisia zako, matatizo yako ya nyumbani yanaweza kusababisha utendaji mbovu kazini. Kila mtu ana matatizo yake anayotakiwa kuyashunghulikia huko nyumbani kwake, lakini utofauti unakuja pale ambapo unaamua kuyaacha nyumbani au kuyaleta ofisini.

9) Unakuwa kilaza/Boya wa ofisi:

Kuna wale watu ambao hula hawana juhudi katika kazi, wanataka watengenezewe vyeo bila kufanya kazi kwa juhudi na utawajua tu kwa matendo yao, hutumia muda mwingi kwenye chai au chakula cha mchana, huja wamechelewa kazini na mara nyingi muda wao wa kukaa ofisini ni mdogo sana , na hiyo kwao ni tabia. Kama siku zote huwezi kufanya kazi ikaisha bila kuwapelekea wenzako wakusaidie ili iishe inawezekana ni muda wako wa kufukuzwa kazi.

10) Wewe ni mtumiaji mbaya wa mali za kampuni au barua pepe:

Mwisho wa siku namna yoyote utakavyotumia vibaya mali za kampuni vinaweza kuhatarisha kazi yako. Kama unatumia laptop(tarakishi mpakato) kwa matumizi yako binafsi kwa ajili ya kupata filamu mpya n.k uwe makini kwani hata barua pepe ni mali ya kampuni hiyo hutakiwi kutumia vibaya.

11) Una mazoea mabaya au mlevi

Sahau kwamba kama unabeba pombe kwenda kazini hiyo ni mbaya zaidi, bali kinachozungumzwa hapa ni kufika ofisini ukiwa katika hali ya uchovu unaotokana na ulevi au mazoea ya kulewa kila wakati, kumbuka kwamba siku moja watu watakushtukia. Kwa sababu yoyote utakayofukuzwa kazi au unahisi kuachia ngazi mwenyewe ila tafuta sehemu ambayo utaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ya kutosha na kutoa matokeo bora zaidi. Inawezekana ni wakati wa kutafuta sehemu bora zaidi na ambapo utaonyesha matokeo bora zaidi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents