Burudani

Kendrick Lamal awachonganisha Wanafunzi na Drake

Baada ya Kendrick Lamar kuanza Tour yake kwa mwaka 2024, alianza kuifanyia nyumbani alipozaliwa Los Angeles California siku ya Ijumaa.

Kwenye Tour hiyo alitumbuiza wimbo wake wa NOT LIKE US aliomdiss DRAKE na baada ya hapo wimbo huo umeanza ku-trend upya kama mpya vile.

Moja ya clip inayosambaa mitandaoni ni hii ikiwaonyesha wanafunzi kwenye moja ya Shule huko Marekani wakiimba kwa hisia na vibe la hali ya juu wimbo huo.

Wengi wamejiuliza namna wanafunzi hawa wanavyoimba wimbo huo kwa ufahamu mkubwa licha ya kuwa ujumbe katika wimbo huo unamuongelea vibaya Drake.

Wanafunzi hao walikuwa katika moja ya sherehe na baada ya wimbo huo kuchezwa kila mtu alianza kuimba kwa sauti kubwa.

Ikumbukwe siku ya Jumamosi Snoop Dogg alimtaja Kendrick Lamar kama ndio Mfalme wa West ( Mfalme wa Marekani Magharibi) wa kizazi hiki.

Hii ingekuwa Kibongo bongo imekaaje?? Ni sahihi au Wanafunzi walikosa cha kufanya??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents