Habari

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe atangaza kushinda urais kabla ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa

Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha MDC nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa ametangaza kushinda uchaguzi uchaguzi mkuu nchini humo kabla ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa rasmi na tume ya uchaguzi.

Image result for nelson chamisa
Nelson Chamisa akipiga kura siku ya Jumatatu iliyopita.

Chamisa kupitia ukurasa wake wa Twitter jioni ya leo amesema anawashukuru watu wote waliompigia kura kwani wamefanikisha yeye kushinda uchaguzi huo na kwa matokeo hayo ya watu wengi yameonesha kuwa wanataka mabadiliko ya nchi yao.

Wakati hayo yakijiri nchini humo, tayari watu wanne wafuasi wa vyama vya upinzani wameuawa na wanajeshi wakati wa maandamano asubuhi ya leo wakiishinikiza Tume ya Uchaguzi nchini humo kutangaza matokeo.

Matokeo ya awali yanaonesha Chama tawala cha ZANU-PF kinachoongozwa na Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa kinaongoza mpaka sasa kwa kushinda viti 110 huku MDC kikijizolea viti 40 pekee.

Wananchi nchini Zimbabwe walipiga kura siku siku ya Jumatatu Julai 30, 2018 kuchagua Rais na Wabunge  katika uchaguzi mkuu wa kihistoria kwenye nchi hiyo iliyotawaliwa na Mzee Mugabe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents