Burudani

Kura za uchaguzi mkuu Nigeria bado zinahesabiwa, Harmonize aandaa show ya kuwapoza machungu mashabiki wake nchini humo

Jana Februari 23, 2019 mamilioni ya watu nchini Nigeria walishiriki katika zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu baada ya shughuli hiyo kuahirishwa ghafla wiki iliyopita.

Image result for buhari vs atiku

Mpaka sasa bado shughuli shughuli ya kuhesabu kura inaendelea na matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutangazwa kesho Jumatatu.

Kwenye uchaguzi huo, Wagombea wawili wakuu ni Rais Muhammadu Buhari, (76) na aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa zamani, Bilionea Atiku Abubakar (72).

Wakati homa ya matokeo ikipamba moto, Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize kesho Jumatatu Februari 25, 2019 ameahidi kutumbuiza nchini humo, kwenye show aliyoiita RELEASE PARTY.

Show hiyo itakuwa mahsusi kwa uzinduzi wa EP yake ya AFRO BONGO na pia itapoza machungu ya uchaguzi nchini humo hususani kwa mashabiki wake.

Show itafanyika jijini Lagos katika ukumbi wa Folixx Lounge na watu watakaoingia watapata shavu la kusikiliza EP hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa hiyo kesho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents