Habari

Kwanini biashara yako itakufa usipokuwa makini

Biashara ni uwezo wa kuuza na kununua bidhaaa au huduma fulani kutoka kwa mtu binafsi au shirika fulani kwenda kwa mtu au shirika jingine. Kila mtu anaweza kuwa na wazo la biashara na akaamua kuanzisha biashara fulani, ila uwezo wa biashara hiyo kusimma unategemea mambo ya msingi kuzingatiwa.

Kitu cha kwanza , je unajua Biashara yako unataka ifike wapi?

Unatakiwa kuweka mpango wako vizuri, ujue malengo ya biashara hiyo na namna utakavyoiendesha.  Ukishindwa kuja malengo na kwanini umeanzisha biashara hiyo utajikuta ukifanya vitu vingi kinyume na biashara ambayo ulitarajia. Si ajabu umekutana na biashara nyingi mtaani mtu akiwa ameorodhesha vitu vingi sana kiasi kwamba unajiuliza je unaweza kufanya hayo yote? Ukweli ni kwamba hawezi vitu hivyo vyote, kuna vitu atavifanya vizuri na vingine hatafanya vizuri na kujiharibia jina.

Usipokuwa na bidhaa inayoshikiria Biashara.
Bidhaa au huduma inayoshikilia biashara, inamaanisha kiini(mhimili wa biashara yako) cha biashara yako ni nini? Je umewekeza sana kwenye nini na una wataalamu au wewe ni mtaalamu wa jambo hilo? Ogopa kuwa mtaalamu wa kila kitu, utakuja kugundua hujui kitu, namaanisha usifanye kila kitu au kila  biashara. Utapotea kirahisi katika malengo ya biasharan akushindwa kuimarisha biashara yako.

Kushindwa kutoa huduma inayostahiki.
Jambo jingine ambalo litaua biashara yako ni kushindwa kumhudumia mteja kwa mategemeo anayohitaji. Mteja ni uhai wa biashara yako, hivyo unatakiwa kuwa makini namna unavyomhudumia na bidhaa yako kushindwa kufanya hivyo ni kujiua mwenyewe. Siri ni hii watu wengi wakianza biashara huanza na huduma bora au bidhaa bora lakini wakipata wateja wanapunguza ubora na huduma zinaanza kuzorota. Je unategemea nini?

Kutozingatia taaluma kwenye biashara yako.
Watu wengi hawazingatii weledi katika biashara , kuwa na wazo la biashara haimaanishi unaweza kufanya hiyo biashara bila msaada wa watu wengine. Unahitaji watu waliosemea hicho kitu kukushauri namna ya kufanya na sio namna ambayo umeona watu wanafanya. Uwe mbunifu na kuongeza taaluma ya kitu unachofanya ili kuboresha biashara hiyo, kushindwa kufanya hivyo biashara yako haitakuwa  kiwango kinachohitajika kibiashara. Zingatia kutafuta masoko, kutangaza biashara yako na utumie teknolojia iliyopo kimawasiliano ili kuboresha huduma yako.

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents