Habari

Kwanini hutakiwi kunywa pombe na bosi wako

Ni sawa kunywa pombe na bosi wako? Kwa hali ya kawaida inaweza kuonekana ni vizuri na haina shida, hiyo ni nadharia tu.  Ukiingia kwa undani zaidi unaanza kumfahamu zaidi kwamba kuna kitu unatakiwa kukijua na kufikiri kwa makini. Unapovuka mipaka kwa kunywa bombe na bosi wako au kwenda sehemu maeneo ya starehe na yeye, unatengeneza mwanya wa kupoteza kazi au kutiliwa mashaka utendaji wako na ufanisi wako kazini.

woman-drinking-with-man

Kumbuka kazi ni kazi haijalishi mlikuwa na muda mzuri kiasi gani jana usiku, hivyo mategemeo yako kazini lazima yabaki palepale. Malengo ya kampuni hayajabadirika kwa wewe kunywa na bosi wako. Kama una urafiki na bosi wako ni vizuri lakini ukishindwa kuwa makini katika urafiki wenu kama inavyotakiwa iwe unajiweka matatani. Inakubidi uwe makini;

1. Kilevi kinakupa ujasiri, hivyo ni rahisi kufanya au kusema ujinga

Kama unafikiri pombe haina madhara, inawezekana. Tunachokizungumzia unakunywa moja baada ya nyingine na wafanyakazi wenzako pamoja na bosi wenu huwezi kujua baada ya kuendeleea kunywa vitu gani utaviongea kwa bahati mbaya na kukuumbua wewe jinsi ulivyo. Baada ya hapo siwezi kusema matokeo take yatakuwaje? Majibu unayo!

Inapotokea mnakwenda kwenye starehe na wafanyakazi wenzako hasa ambao wako juu yako, usijaribu mazungumzo ambayo yatavuka mipaka yako kikazi, funga mdomo wako kwa kadri unavyoweza. Kwa mazingira mengine yanaweza yakasababisha kunyanyashwa kingono kwa wanawake na mahusiano yenu kikazi yakaharibika na wewe kupoteza utu na heshima yako.

2. Unapoingilia maisha binafsi ya mtu ni rahisi kuharibu kazi

Marafiki wanahitaji kutoka na wewe lakini linapokuja suala la taaluma na kazi yako hiyo ni biashara tosha ya kuharibu au kujenga pale ambapo unaruhu mazingira ya starehe hasa pombe na bosi wako.  Weka urafiki wenu kitaaluma zaidi itakujengea heshima na utu wako hata utakapokua unaondoka kwenda kwenye kampuni nyingine.

3. Unajenga mazingira ya upendeleo ambayo wafanyakazi wenzako kukutilia mashaka.

Unaweza kuwa na urafiki wa karibu sana na bosi na bosi wako hasa wakati wa wikiendi, ila itakujengea mazingira magumu kufanya kazi na wenzako ambao hawana urafiki na bosi huyo kama wewe hivyo kuonekana wewe ni mtu wa kutiliwa mashaka kwakuwa hawajui hula mnaongea nini na bosi huyo. Hakuna mtu ataendelea kukwamini ni sawa na kusaliti wafanyakazi wenzako katika kitengo chenu.

Jambo la msingi ni kuwa makini unapokuwa na watu waliokuzidi hasa vyeo, wanahitaji kujua vitu vya msingi kuhusu wewe na sio kila kitu. Kazi kwako!

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents