Habari

Lema aendelea kuhoji tukio la Lissu ‘nani aliwatuma washambuliaji?’

Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema ameendelea kuhoji tukio la  kushambuliwa kwa risasi kwa Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe Tundu Lissu kwa kusema nani aliwatuma washambuliaji huku akihimiza Watanzania kutokubali kukaa kimya juu ya tukio hilo.

Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema

Mhe. Lema amesema kwa sasa kuna mikakati inaundwa na watu ili kuyumbisha mijadala ya tukio hilo la kushambuliwa kwa Lissu lakini amedai kamwe hatoyumba ataendelea kuhoji.

Kuna mkakati kuondoa mjadala wa tukio la Lissu , tusikubali kuondoka ktk mjadala huu .Nani aliwatuma washambuliaji na ni wakinani ?“,ameandika Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

SOMA ZAIDI – Mhe. Spika nashukuru kwa msamaha wako wa bure – Lema

Mhe. Lema ni moja ya Wabunge wa CHADEMA waliopo nchini Kenya kwa ajili ya kumuuguza Mhe. Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu mkoani Dodoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents