Burudani

Madam Rita awacharua wanaosema ‘BSS’ hailipi washindi wake

Kumekuwa na maswali mengi miongoni mwa wafuatiliaji wa shindano la kusaka vibaji Tanzania lijulikanalo kama Bongo Star Search kuhusu uhalali wa zawadi ya milioni 50 kwa washindi wake, huku wengi wakidai kuwa pesa hizo hazilipwi zote kwa washindi.

Rita Poulsen

Sasa Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen ameweka wazi tuhuma hizo kwa kuwacharua watu wanaohoji uhalali wa utoaji wa zawadi ya milioni 50 kwa kuwambia ni chuki zao tu kwani wengi wao hawajawahi kukamata hata milioni 10.

“Hii show ipo kwa miaka kumi unategemea mimi na own nchi, unafikiria kwamba hiyo ishu ingekuwa ipo hivyo BASATA ingekuwa haijawahi kufungia Bongo Star Search, watu hawana sehemu ya kwenda kushitaki? kwanini hamuwaiti hapa mkawauliza, nyinyi mnaona kwamba ni kitu hakiwezekani mtu kutoa milioni 5o, kwangu its very easy roho yangu ipo hivyo, kwa hiyo wote hakuna hata mtu mmoja hajawahi kupata hela yake milioni 50,”amesema Madam Rita na kuanza kuwacharua watu wanaohoji mkanganyiko wa utoaji wa zawadi hiyo.

SOMA ZAIDI – Nay wa Mitego ashangaa kuona washindi wa BSS wakipigika licha ya kulipwa fedha nyingi

Tanzania hii mtu atakuwa hajapewa hela zake tuendelee kuwepo BSS iende mwaka wa tisa mwaka wa ngapi, hii nchi ni ya kwangu? hayo ni maswali ya kijinga“,amesema Madam Rita huku  akisisitiza kuwa “Hao wanaosema hivyo wanawaonea wivu, they are just haters, watu wamepata hela zao, huyo aliyeuliza utakuta hajawahi kushika hata milioni 10,“amemjibu mdau  aliyehoji uhalali wa zawadi ya milioni 50 kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents