Habari

Mambo 10 kuhusu maisha ambayo ni ya kweli lakini tunayapotezea

Kuna masomo magumu ya Maisha ambayo tunajifunza utotoni halafu yanaanza kutoweka katika mawazo yetu pale tunapoendelea kukua. Kushindwa kwetu kujua haya inabakia ni agenda ya kitaaluma zaidi.

image

Kama binadamu tunapenda mawazo ambayo yanaingia akilini mwetu tu na wakati mwingine kukataa vitu ambavyo havikwepeki. Hapa kuna mambo kumi yenye ukweli kwako na yatatokea au yapo kwako ambayo hutoweza kuyakwepa.

Unatakiwa kujua kwamba Utakufa

Unahitaji kutambua kuwa una maisha ambayo yatakoma kwa muda fulani. Hivyo kutusaidia kufanya yaliyo ya msingi na kusahau vitu ambavyo si vya msingi. Vile vile inatusaidia kufanya maamuzi kwa kina na kujua madhara ya maamuzi hayo kila siku. Swali la kujiuliza je nitafanya nini endapo nina miaka mitano tu ya  ya kuishi?

Kila Kitu kina Mwisho wake

Mara nyingi tunaendelea kutafuta furaha au maisha mazuri bila kuwa na kiasi au kuridhika tukifikiri hakuna mwisho. Maisha yanaendelea marafiki zetu tuliokuwa nao wakati wadogo wametoweka au kugawanyika na wengine hatujui waliko.Makampuni makubwa tuliyoyajua yamefirisika na mengine yameibuka. Hivyo tunatakiwa kukubaliana na mabadiliko yanapokuja tukijua tu kwamba hakuna kitu kisichokuwa na mwisho wake hivyo huo mwisho unapokuja tafuta namna ya kukubali na kuendelea mbele.

Hakuna anayejua hatima yake huko siku za Usoni

Tunajipanga na kukuza biashara zetu au kupandishwa cheo au kufanya hiki na kile. Kitu ambacho unatakiwa kujua ni vigumu kujua kwa usahihi kesho itakuwaje ila tilia mkazo na fanya kwa umakini unachofanya sasa na unachojua sasa na uruhusu kukabiliana na vitu usivyovijua vinapokuja. Swali ya kujiuliza je nimekutana na mambo ya kushangaza au hata ya hatari au kufurahisha?

Wakati Huu ndio kitu pekee ulichonacho

Wengi hufikiria sana kuhusu mambo yaliyopita na kuhuzunika kuhusu hayo au kufikiri sana kuhusu mambo ya mbeleni na unasahau kwamba ulichonacho wewe ni sasa. Hivyo si kwamba hutakiwi kufikiri kwa yajayo bali tulia na kuwaza unafanya nini sasa? Tunapoteza muda mwingi kufikiria yaliyopita na kusahau kwamba fulsa tuliyonayo ni sasa na tunaitumiaje?

Huwezi kufanya kila Kitu

Sisi sote tuna muda fulani unakwisha na tunavitendea kazi vichache na tuna uwezo wa kusikilza kwa umakini katika vitu vichache hivyo unahitaji kukubaliana na kuchagua kwa umakini kitu gani unataka kufanya au kitu gani ufanye.

Kuna vitu vingi huvijui

Mara nyingi tumechukua baadhi ya filosofia na kuzishikilia tukiamini tunajua sana lakini wakati mwingine tunajikuta zinatubana na kututesa kifikra. Hivyo tunajifanyisha kwamba sisi ni watu wa aina fulani lakini si hivyo na wakati mwingine tumeangukia papaya na hatuwezi kusema kwa sababu moja ama nyingine tuliwaambia watu wengine kwamba tunajua kila kitu. Je kuna kitu ambacho unafikiri unakijua sana? Hebu fanya utafiti kuhusu hicho kitu halafu uone kama unajua?

Hautajifahamu vya kutosha mpaka Unakufa

Huwa tunafikiri tunajijua vizuri na tabia zetu na misimamo yetu. Ukweli ni kwamba tuko kwenye mchakato wa kujitambua mawazo hasi huondoka pale unapoanza kuingiza mawazo chanya. Tabia zinaweza kubadilishwa, Imani kuangaliwa upya, na hisia zinaweza kukomazwa. Swali jiulize je unajitahidi kuwa kitu fulani kuliko vile ulivyo?

Wewe si bora kuliko mtu mwingine

Najua tunafundishwa kujiamini na kujiona bora na mwenye thamani kuliko watu wengine. Maisha sio ushindani kinachojalisha ni uzoefu kwenye maisha. Hivyo jifunze kujifanyia tathimini kwa vigezo sahihi, ni vizuri ujitahidi kuwa bora kuliko kufikiria kuwa bora zaidi ya fulani. Hebu jiulize huwa unajisikiaje uisipojilinganisha na watu wengine?

Wewe sio wa pekee sana

Ni ngumu kukubaliana kwamba watu wengine hawakuoni kwa jinsi unavyojiona mwenyewe. Kila mtu ana mambo yake ambayo anayawekea kipaumbele ambavyo vinatakiwa kuwekwa mezani kunapokuwa na majadiliano yoyote. Ukijua jambo hili utatengeneza mahusiano na watu kwa kuwaheshimu kama binadamu mwenzako kuliko kufikiria kuwatumia au wakusuduju uonekane bora kuliko wao. Je ninatafuta mahusiano ya kuniridhisha?

Kushindwa ni maamuzi yako mwenyewe

Tunapopanga mipango na kutokea kwa hicho tunachokipanga inategemea njia sahihi ya kutekeleza mipango hiyo. Ila mambo yanapoharibika ,yanakuwa magumu na kuwa ukweli mgumu, je kitu gani kinatokea? Watu wanaofanikiwa kwenye mipango yao wameshindwa kwenye vitu vingi na kujifunza kwa kutafuta suluhisho ya kile walichoshindwa. Huwezi kusema kwamba wewe ni wa kushindwa tu lakini unaweza ukajifunza na kuendelea mbele. Je huwa unajiuliza unaposhindwa?

Kati ya mambo hayo hapo juu, je ni mambo gani kwako ni tatizo? na unafanyaje kupambana nalo?  

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents