HabariMichezo

Mandonga amchapa bondia wa Uganda na kutwaa taji

Bondia machachari na mwenye mbwembwe nyingi mtanzania, Karim Mandonga amechampa Mganda Kenneth Lukyamuzi na kutwaa ubingwa wa PST uzani wa Light-Heavyweight.

Mandonga ameshinda kwa pointi katika pambano hilo la raundi 8 na kutwaa ubingwa huo wa kwanza kabisa katika Maisha yake ya ndondi aliyoanza chini ya miaka 10 iliyopita.

Katika pambano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kasarani huko Kenya lilionekana kama kumuendea vizuri Mganda Lukyamuzi lakini baada ya ushindi Mandonga alisema. ‘Hii game mungu kamsaidia mpaka kafika raundi ya 8 lakini ilikuwa anakufa’.

Ni mara ya pili Mandonga anashinda nje ya nchi katika ardhi ya Kenya, ambapo Januari mwaka huu alimchapa bondia mkongwe wa kenya Daniel Wanyonyi na kuendeleza tambo zake katika ndondi Afrika Mashariki.

Hili ni pambano lake la 5 anashinda mfululizo na kuanza kuonekana kama bondia anayepigana kwa mdomo lakini anapigana ngumi pia, baada ya awali kuonekana ni bondia wa masihara, na anayekubali vichapo kila wakati.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents