Habari

Marekani inahofu kuwa Urusi inaimarisha silaha zake, baada ya kudai imeanza majaribio ya silaha za nyuklia zisizo na nguvu kubwa

Marekani inahofu kuwa Urusi inaimarisha silaha zake baada ya kudai imeanza majaribio ya silaha zake za nyuklia eneo la Arctic

Huenda urusi inakiuka mkataba wa nuklia kwa kufanya majaribio ya silaha za nyukilia zisizo na nguvu kubwa katika eneno la Arctic, Afisa wa juu wa intelijensia wa Marekani ameeleza. Luteni Jenerali Robert Ashley, Mkurugenzi wa taasisi ya intelijensia ya Marekani, amesema Moscow ”pengine inakiuka ” sheria za mkataba.

Alikua akimaanisha mkataba wa pamoja wa Comprehensive Test Ban Treaty (CTBT) unaozuia majaribio ya nuklia.

Kwa mujibu wa BBC. Urusi, ambayo ilitia saini mwaka 2008, inasema inaunga mkono mkataba wa CTBT.

Marekani imetia saini lakini haijaanza kutekeleza mkataba huo.

”kwa uelewa wetu uendelezwaji wa silaha za nuklia unatusababisha tuamini kuwa shughuli za majaribio ya Urusi zitasaidia kuboresha uwezo wa silaha za nyukilia,” alisema Luteni Jenerali Ashley.

Ameongeza kuwa Marekani ilitegemea Urusi, ambayo amesema ilikua inategemewa kujaribu silaha zake katika visiwa vya Zemlya, ili kuongeza ubora wa silaha za nuklia kwa kipindi cha muongo mmoja ujao.

Lakini wachambuzi wa mambo wamepokea taarifa hiyo ambayo hata hivyo haikuwashawishi. Shirika linalosimamia utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa nyukilia CTBTO imesema kwenye taarifa yake kuwa haishuku shughuli zozote zinazokwenda kinyume na mkataba.

CTBT, ambao inapiga marufuku majaribio ya silaha za nyukilia popote pale duniani, ulifikiwa na Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa mwaka 1996.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents