HabariMichezo

Mashabiki wa kike wa Man United kuandamana, hawamtaki Greenwood

Ni takribai msimu wa pili sasa Mshabuliaji wa Manchester United Mason Greenwood yupo nje ya uwanja baada ya kukutana na sakata la kumpiga mpenzi wake Heriot kwa mambo yao ya kimahusiano.

Taarifa ya polisi ilieleza kuwa mchezaji huyo alitaka kubaka na kuua ingawa mapema 2 Feb 2023 alisadikika yupo huru baada ya mahakama kuamuru kuwa mchezaji huo hana kesi ya kujibu baada ya kukosekana ushahidi upande wa pili ambao ni uapnde wa mwanamke.

Taarifa ya mahakama haikuweka wazi kama hana kosa bali walieleza tu hakuna sapoti kutoka upande wa mashataka ambao ni uapnde wa mwanamke wake.

Baada ya taarifa hiyo miezi kadhaa ilielezwa kuwa tayari Greenwood na mpenzi wake wanatarajia mtoto na miezi miwili iliyopita walipata mtoto na mpenzi wake huyo aliyempiga.

Baada ya taarifa ya mahakama ilielezwa kuwa Greenwood atareje tena uwanjani tenna kuichezea Man United.

Leo hii kwa mujibu wa Jarida la The Athletic imesambaa barua ya wazi inayoeleza kuwa mashabiki wa kike wa Man United wataandamana kupinga kurejea kwa mchezaji huo.

Kundi hilo la mashabiki wa jinsia ya kike wa Manchester United, wamepanga kuandamana ili kupinga vikali uamuzi wa klabu hiyo kumrejesha Mason Greenwood kikosini. Waandamanaji hao, ambao pia ni wahudhuriaji wa michezo mbalimbali ya United, wamenuia kuweka hisia zao wazi siku ya jumatatu kabla ya mechi ya ufunguzi wa msimu ambapo United watacheza dhidi ya Wolverhampton Wanderers, Old Trafford.

Tayari mashabiki hao wametengeneza Bango lenye ujumbe usemao “Mashabiki wa Kike wanapinga kurejea kwa Greenwood – Tokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake.” na wamepiga picha nje ya uwan ja wa klabu hiyo Old Trafford.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents