Habari

Mganga aua mfanyakazi wake, Baba wa Maganga auawa pia (Video)

Mlinzi adaiwa kuuawa na bosi wake

Bongo5 ilipokea taarifa kuwa kuna mauaji yametokea eneo la Kigogo Fresh Kama unaenda Chanika ambapo kijana mmoja anaefahamika kama Taz Genius akidaiwa kumuuwa mlinzi wake Jafazi kwa kumpiga na kitu kizito nyuma ya kichwa hadi kifo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa kaka wa Marehemu amedai mdogo wake huyo alikuwa kwenye mgogoro wa kulipana mshahara na bosi wake huyo ambaye ni mganga wa kienyeji.

Amedai baada ya mdogo wake kudai mshahara wake, Taz alikuja na madai kwamba anamdai kijana huyo mashine mbili za kamali ambazo alidai ziliibiwa nyumbani hapo.

Mganga huyo anadaiwa alimshikilia kijana huyo kama mateka katika ghorofa lake mpaka arudishe mashine hizo lakini baada ya jitihada za ndugu aliachiwa mpaka alivyoitwa tena na bosi wake huyo siku jana ambapo leo umauti umemkuta.

Baada ya mganga huyo kudaiwa kutelekeza shambulio hilo pamoja na wenzake anadaiwa kutorokea kusikojulikana ambapo watu wenye hasira walivamia nyumbani kwake na baada ya kumkosa imasemekana wamemuua baba yake mzazi katika hali ya kulipiza kisasi.

Taarifa hizo zinaenda mbali zaidi kwa kudai kwamba mganga huyo wiki mbili zilizopita alishikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa mgonjwa kufariki akiwa nyumbani kwake.

Bado Bongo5 inaendelea kufanya jitihada za kuzungumza na Kamanda wa Polisi kuhusu taarifa hizi.

Kuangalia full interview tembelea YouTube ya BongoFive

Written by @yasiningitu

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents