Habari

Mhe. Zitto Kabwe anyimwa dhamana, Apelekwa mahabusu Morogoro

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe jana usiku alikamatwa na kuchukuliwa maelezo katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro, ambapo baada ya maelezo hayo yaliyodumu kwa saa moja alipelekwa mahabusu kwa kunyimwa dhamana.

Mhe. Zitto Kabwe

Polisi wanaituhumu ziara ya chama cha ACT Wazalendo kutembelea madiwani wao katika kata mbalimbali kwenye mikoa 8 nchini kuwa ni kosa kisheria.

Soma zaidi – Mh. Zitto kufanya ziara Kata zinazoongozwa na ACT Wazalendo

Kwa mujibu wa maelezo ya Wakili  wake, Mhe. Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Baada ya kuandika maelezo Zitto akiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula, Maelezo ysliyoanza saa Saa 4:42 usiku wa jana, mpaka saa 5:40 usiku, Jeshi la Polisi limekataa kumpa dhamana na kumpeleka mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro.

Wakili Mvula amesema pia Jeshi la Polisi limekataa kusema kama dhamana ipo wazi au la, au kuweka wazi masharti ya dhamana.

Soma taarifa iliyotolewa na Wakili wa Zitto Kabwe kwa vyombo vya habari;

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto Zuberi amechukuliwa maelezo katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro, Polisi wanaituhumu ziara ya chama cha ACT Wazalendo kutembelea madiwani wao katika kata mbalimbali katika mikoa 8 nchini kuwa ni kosa kisheria.

Hivyo, ndugu Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Lakini kosa hilo amefunguliwa peke yake tu.

Baada ya kuandika maelezo akiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula, tokea saa Saa 4:42 usiku wa jana, mpaka saa 5:40 usiku, Jeshi la Polisi wamekataa kumpa DHAMANA kwa maelezo wanasubiri maelekezo toka kwa wakubwa wao. Hivyo ndugu Zitto amewekwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro.

Pia Jeshi la Polisi limekataa kusema kama dhamana ipo wazi ama la, na kama ipo wazi masharti yake ni yapi, na wamekataa pia kusema iwapo leo watampeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria au la.

Emmanuel Lazarus Mvula
Wakili wa ndugu Zitto
Morogoro
Februari 23, 2018

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents