Habari

Mimi sio kilaza – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewatahadharisha viongozi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro kuwa wawe makini na matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kukarabati miundo mbinu chuoni hapo.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Magufuli amesema kuwa yeye sio ‘KILAZA’ katika ufuatiliaji wa miradi ambayo serikali yake inatoa fedha kwa hiyo amewaomba viongozi hao wahakikishe fedha hizo zinazotolewa na serikali zinafanya kazi iliyokusudiwa.

Tatizo langu mimi ni moja tu, ni kwenye usimamizi, nimeenda Mkwawa nimekuwa soo much discouraged, sitaki chuo hiki kini-disdiscourage sipendi ninapotoa hela na bahati mbaya mimi ninafuatilia. Mimi sio kilaza katika kufuatilia ninafuatilia kila senti, na ninafahamu value for money ,”amesema Rais Magufuli leo Mei 07, 2018 alipotembelea Chuo cha Sokoine (S.U.A) mkoani Morogoro baada ya kuagiza kiasi cha bilioni 2 zilizotengwa kutumika katika chuo kikuu UDSM zipelekwe chuoni hapo kwa ajili ya kujenga mabweni.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewaasa wanafunzi waache tabia ya kujihusisha na masuala yaliyo nje na masomo wakiwa shuleni kwani katika awamu hii ya uongozi wake hatawavumilia wanafunzi wa aina hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents