Habari

Moja ya majengo marefu zaidi China SEG Plaza, limezua hofu baada ya kutikisika (+ Video)

Watu waliokuwa ndani ya Jumba refu lenye ghorofa 70 nchini China wameondolewa baada ya jumba hilo kuanza kutikisika. Hatua hiyo iliwafanya watu waliokuwa ndani yake kutoroka wakihofia maisha yao katika mji wa kusini wa China Shenzhen.

Maafisa tawala wa eneo hilo hawajui kilichosababisha jumba hilo lenye urefu wa mita 300 la SEG Plaza kuyumbayumba siku ya Jumanne mchana .

Hakuna tetemeko la ardhi lililorekodiwa wakati huo .Uchunguzi unaendelea.

Jumba hilo la miaka 20 linamiliki soko la bidhaa za elektroniki na afisi. Lipo katika mji wa Shenzhen , mji unaochipuka wa watu milioni 12 likisifika kuwa soko la bidhaa hizo za kiteknolojia.

Kanda za video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zilionyesha mamia ya watu wakilitoka jumba hilo muda mfupi walipoambiwa kutoka.

Gazeti la China Global Times liliripoti kwamba serikali ya eneo hilo la wilaya ya Shenzhen Futian ambapo ilipokea ripoti kwamba jumba hilo lilikuwa likiyumba kutoka kwa wafanyakazi waliopo ndani ya jumba hilo mwendo wa saa sita na nusu saa za China. Kufikia saa nane , kila mtu ndani yake alikuwa ametolewa , gazeti hilo liliripoti.

Katika taarifa iliotolewa baadaye , serikali hiyo ilisema kwamba uchunguzi wa mapema ulionesha kwamba hakuna nyufa zilizopatikana katika msingi wa jumba hilo wala hakukuwepo na unaribifu katika kuta zake.

Baada ya ujenzi wake kukamilika 2000, SEG Plaza ndio jumba la 104 kwa urefu nchini China na la 212 kwa urefu kote duniani , kulingana na baraza la majumba marefu na makaazi ya mijini .

Mji wa Shenzhen ambao unaunganisha Hong Kong na China bara, ndio mji uliosheheni bidhaa za teknolojia na uvumbuzi nchini humo.

Biashara zenye makao yake makuu mjini humo ni pamoja na Tencent na Huawei. Jumba la nne kwa urefu duniani la Ping An Finance Center lenye urefu wa mita 599 pia lipo katika anga za mji huo.

Kuanguka kwa majumba sio jambo la ajabu nchini China . Mwezi Mei mwaka uliopita , hoteli moja iliokuwa ikitumika kama eneo la karantini wakati wa mlipuko wa virusi vya corona katika mji wa Quanzhou lilianguka na kuwaua watu 29.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CPC9WYkhLt7/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents