Habari

Mtanzania anusurika kifo baada ya kujifungia kwenye kontena bandarini kwa masaa 23 (+video)

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Hassani Mkazi wa Miembeni mjini Unguja amenusurika kifo baada ya kutolewa ndani ya kontena ambapo alidaiwa kujifungia.

Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa Msimamizi wa makontena katika Bandari ya Malindi, Ibrahim Abdallah kwenye mahojiano yake na gazeti la mwananchi leo Mei 13, 2018 amesema bado sababu ya mtu huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 30 kujifungia kwenye kontena haijajulikana na kwa sasa amepelekwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja mjini humo.

Akielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea, Abdallah amesema wakiwa katika eneo hilo la kazi saa moja asubuhi walisikia sauti ikisema “Nakufaaaa” ikitoka ndani ya kontena na walipouliza wewe ni nani walijibiwa “Hassani”.

“Baada ya kutaja jina tulifungua kontena ambalo alikuwa amelifunga na kumtoa akiwa na hali mbaya kiafya na tulimpeleka Hospitali ya Mnazi Mmoja ili kupatiwa huduma ya kwanza,” amesema Abdallah kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi.

Hata hivyo mashuhuda wa tukio hilo ambao wengi ni wafanyakazi bandarini hapo wamesema haijawahi kutokea tukio kama hilo la mtu kujifungia katika Kontena na makontena hayo yamepangwa tangu jana asubuhi .Tazama video ya tukio hilo la kuokolewa kwa Hassani.(Video na Mtandao)
https://youtu.be/BF9Hc6OVCPI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents