Burudani

Mtoto wa Arnold Schwarzenegger amkataa Baba yake

Mtoto wa Arnold Schwarzenegger, Joseph Baena anatema licha ya kufuata nyayo za Baba yake katika tasnia ya uigizaji na utunishaji wa misuli, lakini hataki kutumia jina la mwisho la Baba yake nyota wa Terminator.

Kwenye mahojiano ya hivi karibuni Joseph alinukuliwa akisema “Nitajaribu kufanya mambo yangu kivyangu”.

Joseph anatumia jina la ukoo wa Mama yake aitwae Mildred Baena, huku akijitengenezea njia yake mwenyewe huko Hollywood.

“Nadhani jambo kubwa hapa ni kwamba ninajaribu kufanya mambo yangu kivyangu, ni muhimu sana kama mwanaume kufanya mambo peke yako”.

Mildred Patricia Baena Mama yake Joseph alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Arnold Schwarzenegger kabla wawili hao hawajaingia kwenye Mahusiano.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents