Burudani

Nimewambia Wasafi TV wacheze nyimbo za Alikiba – Nikki Mbishi (+video)

Rapa Nikki Mbishi ametoa ushauri kwa uongozi wa Wasafi TV kuwa usibadilike siku za usoni bali uendelee kusapoti kazi za wasanii wote bila kuchagua au kuweka matabaka kwenye muziki.

Akiongea na Bongo5, Nikki Mbishi amesema kuwa kituo cha Wasafi TV kimeanza vizuri lakini ameona vituo vingi vya runinga vikianza hivyo halafu baadaye vinabadilika kabisa kitu ambacho ni kibaya kwenye muziki wetu.

Kwa upande mwingine, Nikki Mbishi amesema wiki nzima amekuwa akitazama Wasafi TV na ameona nyimbo tofauti zikichezwa na amedai kuwa amewashauri Wasafi TV wacheze pia hata nyimbo za Alikiba, ingawaje amekiri wazi kuwa kuna watu wataoponda video zake kuchezwa lakini hao watu kamwe hawawezi kukosekana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents