Habari

Ongezeko la walaji wa nyama ya mbwa nchini China lazua taharuki mitaani

Serikali nchini China kupitia wizara yake ya Afya ya Wanyama na Ukaguzi imedai kuwa ongezeko la walaji wa nyama ya mbwa nchini humo kumepelekea ongezeko la kesi za watu kupotelewa na mbwa kuongezeka.

Tokeo la picha la dog meat festival

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la Change.Org nchini China kwa mwaka zaidi ya mbwa milioni 20 huchinjwa kwa kitoweo ambapo inakadiliwa kuwa mbwa milioni 2 huchinjwa kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 ukilinganisha na mwaka 2015.

Serikali ya China tayari imeanzisha msako wa kukagua leseni za bucha zinazotoa huduma ya kuuza nyama ya mbwa ili kubaini ukubwa wa ongezeko la bucha zinazofanya kazi bila kibali maalumu.

Wiki iliyopita maafisa usalama nchini humo walikamata lori lenye mbwa 200 wakisafirishwa bila kibali maalumu na tayari mbwa hao wameshapata wenyewe.

Taarifa hiyo imekuja baada ya maafisa usalama nchini humo kueleza kuwa kuna ongezeko la kesi za watu wakiripoti kila siku kupotelewa na mbwa majumbani kwao.

Tayari wanaharakati nchini China wameungana na nchi nyingine kulaani utumiaji wa nyama ya mbwa kama kitoweo huku wakidai kuwa sio unanyanyasaji wa Wanyama.

Nchini China baadhi ya watu hutumia nyama ya Mbwa kama kitoweo kama sehemu ya utamaduni wao.

Wakati hayo yanajiri, jana mtandao wa kupambana na ulaji wa nyama ya mbwa duniani wa Fight Dog Meat umeripoti kuwa nchini China kuna watu wanawauwa mbwa hao kwa kuwachoma kwa moto wa gesi hadi kufa na kuwafanya vitoweo.

Hata hivyo tayari wanaharakati wameanza kupiga vita tamasha kubwa la ulaji nyama ya mbwa la  The Yulin Dog Meat Festival linalofanyika mjini Yulin nchini China kila mwaka ambapo inakadiliwa zaidi ya mbwa elfu 10 huchinjwa.

Vyanzo – TheFightDogMeat & Change Org

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents