Habari

Picha: Rais Magufuli awaapisha Mabalozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Oktoba 2017, amemuapisha Meja Jen. Issa Suleinam Nassor kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulharaman Kaniki kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Mara baada ya kula kiapo, Balozi Issa Suleinam Nassor amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha imani kwake na kumteua kushika nafasi hiyo na amemuahidi kuendeleza na kukuza uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Misri.

Kwa upande wake Balozi Abdulharaman Kaniki amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumteua kushika nafasi hiyo na ameahidi kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Zimbia ulioasisiswa na Hayati Baba wa Taifa Mw. Julius Kambarage Nyerere na Dkt.Keneth Kaunda.

Balozi Kaniki amemuahidi Mhe.Rais Magufuli kuwa atafanya kazi dhamira ua kuliendeleza Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) ambalo limekuwa kiungo muhimu katika nyanja ya kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

PICHA ZOTE NA IKULU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents