Habari

Rais Magufuli afanya uteuzi huu wa katibu mkuu mpya

Rais Magufuli afanya uteuzi huu wa katibu mkuu mpya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Gerald Musabila Kusaya, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, uteuzi ambao umeanza rasmi leo Machi 5, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli

Katibu Mkuu huyo mpya anachukua nafasi ya Mhandisi Mathew Mtigumwe, ambaye amepangiwa nafasi nyingine katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Ikumbukwe kuwa kabla ya kuteuliwa, Kusaya alikuwa kwenye timu maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kwa ajili ya uchunguzi wa masuala mbalimbali katika tasnia ya zao la Mkonge mkoani Tanga.

By Ally juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents