Burudani

Rapa Cassper Nyovest atangaza hatari mwaka huu, Awapigia magoti MaDj’s

Ukitaja marapa wanaofanya vizuri barani Afrika kwa sasa huwezi kumuacha, Cassper Nyovest kutoka Afrika Kusini ambaye tayari amewatangazia habari njema mashabiki wake kuwa kwa mwaka huu ni mwendo wa kutoa hit juu ya hit.

Tokeo la picha la
Cassper Nyovest

Cassper ambaye ametangaza kuachia ngoma mpya kesho Ijumaa Machi 23, 2018 amesema kuwa kwa sasa muziki wa Hip Hop nchini Afrika Kusini unakosa airtime tofauti na kipindi cha nyuma na kuwaomba MaDJ’s nchini humo waoneshe ushirikiano na wasanii wa muziki ili kurudisha heshima ya muziki huo kama ilivyokuwa zamani.

MaDJ’s wote wa Afrika Kusini tunawaomba muanze kuupa muziki wa Hip Hop kipaumbele kama mlivyokuwa mkifanya zamani, Kuna wakati wote mlifanya hivyo tunataka mfanye hivyo tena. Muziki wetu unafanya vizuri sana nje ya Afrika Kusini, tuamke!,“ameandika Cassper Nyovest kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kauli ya Cassper Nyovest ya kuwaomba Ma’DJ’s kuongeza nguvu ya kupiga nyimbo za Hip Hop nchini Afrika Kusini inakuja baada ya malalamiko ya wadau wa Hip Hop nchini humo kudai kuwa muziki huo kwa mwaka 2017/2018 umeanza kushuka ukilinganisha na miaka ya miwili iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents