Michezo

Rashford ni sawa kupigwa chini – Ten Hag

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amesema Marcus Rashford amestahili kupigwa chini kwenye kikosi cha England kilichokwenda kwenye Euro 2024 huko Ujerumani.

Akizungumza wakati anafanya uchambuzi huko Uholanzi kwenye chaneli ya NOS, akichambua mechi ya England ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Serbia alisema: “Grealish na Rashford wote walishindwa kufanya vyema msimu uliomalizika. Na unaposhindwa kufanya vizuri, basi huwezi kuchaguliwa na timu yako ya taifa.” .

Na alipoulizwa kwanini kiwango cha staa huyo kimeshuka, Ten Hag alijibu: “Ni mjadala unaovutia. Anajua, najua. Ni kitu anachopaswa kukifanyia kazi yeye binafsi, lakini na timu pia inatakiwa kumsaidia. Ni mjadala kwa sababu ni kitu kinachohusisha takwimu.”

Rashford alipigwa faini ya kukatwa mshahara wa wiki mbili baada ya kushindwa kuhudhuria mazoezi kufuatia kukesha akilewa huko Belfast. Fowadi huyo alisafiri kwenda Ireland wakati wa siku ya mapumziko mapema mwaka huu kwenda kumtembelea mchezaji mwenzake wa zamani, RoShaun Williams, anayechezea Larne, na baadaye aliripotiwa kwamba aliugua akiwa kwenye treni.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents