Habari

Rayvanny aachia wimbo maalum wa kukemea vurugu za #Xenophobia nchini Afrika Kusini (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amekuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuachia wimbo maalum wa kukemea vurugu za ubaguzi zinazoendelea nchini Afrika Kusini kati ya raia wazawa na wafanyabiashara wa kigeni.

Kwenye wimbo huo wa ‘AFRICA’, Rayvanny kuna mashairi anasikika akisema “Kama hatutakemea machafuko yanayoendelea, Basi siku moja machafuko yatatumaliza wote”.

Rayvanny pia ametumia nukuu za muasisi wa Taifa la Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela akisema “Watu wanajifunza kuchukia, Na kama wanajifunza kuchukia basi wanaweza pia kujifunza kupenda,”.

Vurugu zinazoendelea Afrika Kusini kati ya wazawa na raia wa kigeni, Zimeibua hisia kali kwa watu maarufu Afrika na duniani kwa ujumla.

T.I, Michael Blackson, Trevor Noah, Wizkid, Tiwa Savage, Burna Boy, Cassper Nyovest ni moja ya watu waliopaza sauti juu ya vurugu hizo.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents