Habari

RC Chalamila ataka bei ya mkaa ipande

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema ili kuondokana na matumizi ya Nishati Chafu, basi ifike mahali bei ya gesi iwe chini na bei ya mkaa iwe juu.

Chalamila amesema hayo leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam ambapo imefanyika hafla ya Uzinduzi wa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia 2024-2034.

Chalamila ameongeza kuwa kutokana na idadi kubwa ya wakazi wa mkoa wa Dar  es salaam kutumia mkaa, yeye ameungana na viongozi wa mikoa mbalimbali katika kutokomeza matumizi ya nishati chafu kwa kuhimiza watu wa mikoani kuacha kukata miti hovyo na wa mkoa wa Dar es Salaam kuacha kutumia mkaa kwa ajili ya kupikia.

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

cc- Tanzaniaweb.Live

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents