Habari

RC Makonda atema cheche kwa Viongozi wanaotukana twitter ‘Tutaona kama twitter zitapiga kura mwakani’ – Video

RC Makonda atema cheche kwa Viongozi wanaotukana twitter 'Tutaona kama twitter zitapiga kura mwakani' - Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi eneo kwa Jeshi la kujenga taifa Suma JKT kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi eneo hili jana Makonda aliwataka Suma JKT kujenga hospitali hiyo kwa muda wa miezi mitatu ili wananchi waweze kupata mapema huduma za Afya.

Siku chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwaajili ya Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ubungo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kukagua eneo itakapojengwa hospital hiyo na kuwaekekeza JKT kuhakikisha wanafanya kazi usiku na Mchana na kukabidhi jengo ndani ya Miezi mitatu kuanzia leo ili wananchi wa wilaya hiyo wapate huduma Bora za Afya.

RC Makonda amesema Hospital hiyo inajengwa eneo la Kimara Baruti kwenye eneo lenye ukubwa wa Hekari 5.5 ambapo amemshukuru Rais Magufuli Kwa moyo Wa Upendo anaoendelea kuonyesha kwa Wakazi wa Dar es salaam na Wilaya ya Ubungo.

Aidha RC Makonda amesema kuwa maandalizi yote ya ujenzi yamekamikika na kazi ujenzi itaanza rasmi kesho huku akibainisha kuwa kukamikika kwa Hospital hiyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza changamoto za Afya Wilayani humo.

Itakumbukwa Juzi October 26 wakati wa hafla ya Kupokea ndege ya 8 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda alitumia hafla hiyo kuwasilisha kilio cha wakazi wa Ubungo juu ya kukosekana kwa hospital ya wilaya ya Ubungo ambapo Rais Magufuli alipokea kwa mikono miwili ombi hilo na Kumuelekeza Waziri wa TAMISEMI kutoa fedha hizo na hatimae leo utekelezaji wa ujenzi unaanza.

Makonda aliongeza “Hawa wanaoishi Twitter tuwaache na maisha yao Twitter, Sisi tunahitaji huduma Twitter haiwezi kukupa Panadol, wanavyojenga hoja kwenye Facebook nani kule mwenyekiti wa Facebook nani mwenyekiti wa kikao cha Twitter, Huwezi kuwa kiongozi unashwindwa kushughulikia maendeleo ya watu unabaki kutukana watu kwenye mitandao, Nawatakia kila la kheri huko Twitter lakini Mwaka huu na mwaka ujao tutaona kama Twitter zinapiga kura”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents