Bongo5 ExclusivesBurudani

RECAP: Bongo fleva ina safari ndefu sana (Video)

BONGO FLEVA INA SAFARI NDEFU LINI WASANII WETU WATAFIKA LEVEL HIZI?? LINI WATAALIKWA NA LOUIS VOITON KAMA WANIGERIA??

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP NA MANDO amezungumzia namna wasanii wa Nigeria wanavyoitikisa dunia kila kona.

@el_mando_tz anasema kuwa Wanigeria kwa sasa wanatamba sana wameiacha Tanzania kimuziki mbali sana na ni taifa ambalo wasanii wake walikuwa linashindana na Tanzania.

Anasema kuwa hiki ni kitu cha kujifunza sana kwa wasanii wetu maana ni sehemu ya wao kwenda kujifunza mambo mengi ya kimuziki.

Wasanii pekee kutoka Tanzania ambao angalau huwa wanashiriki Events kubwa duniani huwa ni Diamond na Rayvanny wengine bado sana.

Lini wasanii wetu watafikia level hizi?? Lini wasanii wetu wataalikwa kwa ukubwa na makampuni makubwa sana hivi duniani??

Kuna namna Bongo Fleva bado ina safari ndefu sana, asilimia kubwa wasanii wetu hawana Exposure kubwa duniani.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents