Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

RECAP: Chris Brown aliwapost Miso Misond ila hakufanya challenge yao – El Mando

RECAP: Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amefafanua kuhusu watu kusema Chris Brown alicheza wimbo wa Miso Misondo.

Mbali na hilo ameeleza kuhusu watu kudai Diamond huenda amemlipa Chris Brown dola 2,000 ambayo ni Tsh milioni 5.2 za Kitanzania ili afanye Challenge ya wimbo wa Komasava.

Kuhusu watu kudai Chris Brown kucheza wimbo wa Miso Misondo amesema sio kweli bali Chris Brown alipost clip iliyokuwa unasikika wimbo wake na kwenye Clip hiyo Watu mitandaoni waliunganisha na video ya Miso Misondo.

Lakini pia kuhusu watu kusema Chris Brown analipwa dola 2000 au milioni tano za Tanzania ili afanye Challenge za nyimbo mbalimbali sio kweli bali Chris Brown alitangaza kulipisha watu wanaotaka kupiga naye picha.

Mbali na hilo @el_mando_tz amesema kushangazwa na wasanii wa Tanzania kuonyesha upando kwa kuipost clip ya Chris Brown akicheza wimbo wa Komasava lakini ushirikiano huo hawakuuonyesha mwanzoni wakati wimbo husika unatoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents