BurudaniHabari

RECAP: Diamond amembeba sana Jux Kimataifa, Ajiongeze – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia Show aliyofanya Diamond Dubai kwenye club ya Blu Club Dubai.

Anasema kuwa Diamond amekuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya Show kwenye club ambayo wasanii wakubwa duniani wameonekana wakienda kufanya show pale.

Ametaja baadhi ya wasanii akisema mfano ni Kanye West, Travis Scott, Lilduk na wengine wengi kutoka Marekani na kila kona ya Dunia, hata ukiingia kwenye page yao ya Blu Club Dubai uataona picha zao.

Mbali na hilo amegusia kuwa Diamond anambeba sana Juma Jux Kimataifa na yeye anatakiwa kujiongeza ili apige hatua Kimuziki Kimataifa.

Kupitia Collabo aliyompa ya Enjoy imemfungulia sana milango na hata kwenye baadhi ya Show tumemuona akipafomu kama Trace Afrika iliyofanyika nchini Rwanda.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima link hii hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents