BurudaniDiamond PlatnumzHabari

RECAP: Jason Derulo ana ushawishi mkubwa mitandaoni

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia kuhusu Collabo ya Diamond Platnumz na Jason Derulo ambayo @s2kizzy amethibitisha ipo tayari.

Mbali na hilo amejaribu kumzungumzia Jason Derule na faida itakayopatikana kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva endapo collabo yao itatoka kweli.

Kumbe Diamond alim-DM Jason Derulo mwaka 2021 na DM ikajibiwa mwaka 2024 😳

Pia amewajibu watu wanaojaribu kumdogosha Jason Derulo kwa kusema Jason Derulo ni msanii wa kawaida, @el_mando_tz amemzungumzia kwenye upande wa ushawishi mitandaoni kwa kutaja numbers zake kwenye platform za muziki yaani Viewers na Streams/Plays.

Ameongeza kuwa mbali ya DM ya Jason Derulo wasanii wengi wa Bongo Fleva wamekuwa wakipost DM za wasanii wa Kimarekani lakini Collabo hazitokagi.

Anahoji kuwa kwanini wanakuwa wanawadanganya mashabiki?? Imekuwa kama fashion kwa wasanii wengi sasa na inaanza kukera.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents