Bongo5 ExclusivesBongo5 MakalaBurudani

RECAP: S2kizzy aige kwa Majani na Master Jay (Video)

RECAP: MAPRODUCER TZ HAWAJUI THAMANI YAO, S2KIZZY AIGE KWA MAJAN NA MASTER JAY, WASIHONGWE MAGARI NA WASANII.

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia namna Maproducer Tanzania wasiojua thamani yao kuhusu kazi wanazozifanya.

Anasema kwa namna sakata la S2kizzy na Baddest lilivyotokea kupitia wimbo wa SENSEMA imeonyesha ni namna gani Maproducer wanachukuliwa poa.

Kwa asilimia kubwa Maproducer Tanzania hawana nguvu kwenye wimbo wa msanii hada beat bali msanii anakuwa mmiliki wa kila kitu.

Anaongeza kuwa Maproducer Tanzania waige namna P Funk Majan na Master Jay walivyokuwa wanafanya kazi na ndio maana mpaka leo wananufaika tu, wao ndio wamiliki wa Beat ya wimbo na sio msanii.

Lakini pia ametolea mfano namna baadhi ya Maproducer wa zamani wanavyoishi maisha magumu licha ya kufanya kazi kubwa sana ya muziki kwa wasnaii.

Anaongeza kwa asilimia kubwa msanii ndio mfaidika mkubwa wa wimbo kuliko msanii na ndio maana Msanii akifanikiwa humpa zawadi ya gari Producer kitu ambacho sio sawa.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo kwenye akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents