BurudaniHabari

RECAP: Kwanini wasanii wa Tanzania sio washindani kimuziki Afrika, hawaijui biashara ya muziki?

Kupitia kwenye kipindi chake pendwa cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amehoji sababu za muziki wa Bongo Fleva kutofanya vizuri katika bara la Afrika kulingana na mataifa mengine kama Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Cameroon na kadhalika.

Amesema kuwa moja ya kitu ambacho kinaua muziki wetu na kusababisha kutofanya vizuri nje ya Tanzania kwa sababu wasanii wanatengeneza muziki kwa ajili ya Watanzania na sio watu wanaozungumza Kiswahili barani Afrika.

Ameongeza kuwa wasanii wetu wamejifungia kwennye sehemu ndogo ya Utanzania badala ya kufanya muziki kwa ajili ya Afrika na watu wanaozungumza kiswahili maana Kiswahili ni miongoni mwa Lugha zinazozungumzwa zaidi Afrika, hivyo ukiwakamata wote wanaoongea Kiswahili tutakuwa mali sana.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents