Habari

Shule ya Islamic Kinondoni yateketea kwa moto, Hii ni mara ya tatu ndani ya miezi miwili

Shule ya Sekondari ya Mivumoni Islamic, iliyopo katika eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni Dar es Salaam, imeteketea kwa moto Alafajiri ya leo Agosti 31, 2020, na kuelezwa kuwa hii ni mara ya tatu shule hiyo kuungua ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Magari ya Zimamoto

Akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio hii leo Kamishina Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni Salum Mohamed, amesema kuwa taarifa ya chanzo cha moto huo itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge.

“Kwa kipindi cha miezi miwili hili ni tukio la tatu katika shule hii, Julai 18 tulipata tukio la moto la muundo huu na tulizima, Julai 23 tukio la moto tena lilitokea hili ni tukio la tatu mfululizo ndani ya eneo moja, ni matukio ambayo yanaendelea kutokea ndani ya hizi Shule za Kiislamu za Jijini Dar es Salaam, uchunguzi umefanyika na Msemaji wa hili ili kujua chanzo ni nini ataitoa Mkuu wa Mkoa ” amesema Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto.

Aidha Kamishina Mohamed amesema kuwa katika matukio yote matatu, hakuna madhara kwa binadamu, bali ni uharibifu wa mali na miundombinu ya Shule hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents