Habari

SportPesa kushirikiana na Vodacom watangaza neema kwa Watanzania

Kampuni ya kubashiri michezo nchini Tanzania ya SportPesa kushirikiana na Mtandao wa Vodacom Tanzania wametangaza promosheni mpya ya ‘JIONGEZE NA M-PESA, SHINDA NA SPORTPESA’ ambapo wateja wao watashindania zawadi ya Bajaj aina ya TVS KING DELUXE zitakazowawezesha kukwamuka kiuchumi.

Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Bi. Sabrina Msuya

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo, Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Bi. Sabrina Msuya amesema kuwa nafasi hiyo ni fursa kwa wateja wa SportPesa na wa Vodacom kwani imewalenga wao.

Hii ni fursa nzuri na kwa wateja wetu wa Vodacom kushiriki kwenye promosheni hii kwa kucheza na Sportpesa ili kujishindia Bajaj mpya za TVS King,“amesema Bi. Msuya .

Bi. Msuya amesema promosheni hiyo imeanza leo Februari 9, 2018 na kila wiki watatoka washindi wawili wa Bajaj na promosheni itadumu kwa wiki 10 ambapo jumla watu 20 watashinda Bajaj hizo.

Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo mteja wa Vodacom unatakiwa kutuma neno GAME kwenda 15888 kujisajili na SportPesa, kisha weka pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa kupitia M-PESA kisha anza kubeti na hapo moja kwa moja utakuwa umeingizwa kwenye droo ya promosheni ya ‘JIONGEZE NA M-PESA, SHINDA NA SPORTPESA’. Tazama maelezo zaidi hapa chini

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents