Habari

Tanzania, Uganda vinara wa nchi zenye wafungwa wengi Wakenya duniani

Serikali ya Kenya kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema kuwa kuna wafungwa 1,300 raia wa Kenya waliofungwa nje ya Kenya.

Balozi CS Monica Juma akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Nairobi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 08, 2018 jijini Nairobi, Waziri mwenye dhamana Balozi CS Monica Juma amesema kuwa Kenya nayo mpaka sasa imeshawafunga raia wa kigeni 2,000 kwa makosa mbalimbali, huku akiahidi kuchukua hatua za kidiplomasia kwa mazungumzo zaidi ili kuweza kubadilishana wafungwa.

“Hili ni jambo la kawaida kuwa na Wakenya katika magereza nje ya nchi kama hatua za kisheria zilifanyika, Serikali yetu imeanza mazungumzo ya kidiplomasia na balozi zetu kwenye nchi husika kuhusu wafungwa 1,300 waliopo nje ya Kenya,’amesema Balozi Juma.

Akitaja nchi zinazoongoza kuwa na wafungwa wengi Wakenya Tanzania imeongoza kwa kuwa na wafungwa 79, Uganda imefuatia ikiwa na wafungwa 47 na Ethiopia ina wafungwa 15 huku wengine wakifungwa kwenye tofauti tofauti.

Soma zaidi taarifa hiyo HAPA .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents