Habari

Tubadili Sheria Sukari isiwe bei – Musukuma

Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheku Musukuma akichangia mjadala wa bajeti kuu ya Serikali unaoendelea Bungeni Jijini Dodoma amewashauri Wabunge wenzake kuangalia namna ya kubadili sheria itakayosaidia kuondoa tatizo la upatikanaji wa sukari Nchini hasa kwa kipindi cha January hadi March.

Musukuma amesema “Tumechoka kuona kila mwaka unapofika mwezi wa kwanza, wa pili na mwezi wa tatu tunaanza kupiga kelele ya sukari haiwezekani, misamaha inatolewa lakini matatizo ni yaleyale na ukienda Zambia mpakani sukari inauzwa bei rahisi, ukienda Mutukula inauzwa rahisi lakini kwetu kila mwaka mwezi wa kwanza, pili na watatu kelele zinaanza humu ndani na Wananchi wetu na Mimi nasema ukweli Wananchi wa Geita vijijini, kijiji cha Izumachele walinunua sukari kwa Tsh. 11,000 na ushahidi ninao sasa hatuwezi kuwa na Nchi ya namna hiyo”

“Lipi bora tuwe na viwanda vya Wanyonyaji kutengeneza kuipiga shoti Serikali Wananchi wakanunua sukari Tsh. 10,000 wakati hapa Mutukula Watu wananunua sukari Tsh. 2800 hivi ni viwanda au ni viwandani?”

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents