Habari

Upigaji ‘selfie’ waongeza idadi ya watalii katika eneo hatari zaidi duniani kulifikia (+picha)

Kwa ulimwengu wa sasa wa mitandao ya kijamii hutashangaa kuambiwa watu wanatafuta maeneo mbalimbali ya kupiga picha na kuweka mitandaoni ili kuwaonesha marafiki zao kuwa nao wapo kwenye ulimwengu wa kisasa.

Sasa takwimu kutoka nchini  Norway zinaonesha kuwa asilimia 60 ya watalii walioingia mwaka huu nchini humo hutembelea katika ziwa Ringedalsvatnet wengi wao wakihitaji kupiga picha za “selfie’ kwenye mwamba mkubwa unaoning’inia katika ziwa hilo.

Mwamba huo unaofahamika kwa jina Trolltunga unaning’inia kwa umbali wa futi 1000 kutoka juu ya ziwa Ringedalsvatnet na watu wengi barani Ulaya huvutiwa na sehemu hiyo kwa ajili ya kupiga picha kwa kumbukumbu.

Bodi ya Utalii nchini humo imesema kuwa Watalii husubiriana kupanda kwenye mwamba huo kwa ajili ya kupiga picha hadi masaa matatu kwa sasa hii ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo wageni wengi walikuwa wakiogopa kupanda kwenye mwamba huo.

Hata hivyo, Bodi ya Utalii imedai kuwa kwa miaka ya nyuma haikuwa rahisi kuufikia mwamba huo kwani watu wengi walikuwa ni waoga lakini kwa sasa hivi hata watoto hupanda na simu zao na kujipiga picha wenyewe yaani ‘Selfie’.

Kwa mujibu wa maelezo ya Muongozaji wa Watalii kutoka Kampuni ya Trolltunga Adventures ya mjini Oslo ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya miamaba, Bwana Kenneth Warvik amesema kuwa watalii hutembea kwa miguu kwa masaa sita kupanda mlima hadi kuufikia mwamba huo.

Hapa naanza kuelewa kwa nini watalii wengi hawaoni taabu kutembea kwa miguu kutoka mjini  Bergen hadi huku milimani, ambapo wengi wao hutumia masaa sita. Sio kwa sababu ya kutalii tu lakini wengi wanapenda picha kwani kundi kubwa ni vijana na huwa wanatembea na kamera, Laptop na wengine simu zao cha ajabu hakuna mtu anayetazama tu na kurudi mjini Bergen bila kupiga picha hii inaonesha kuwa ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii limeleta neema kwa Norway.“amesema Bwana Warvik kwenye mahojiano yake na Daily Mail.

Taarifa kutoka Mtandao wa Shirika la Utangazaji nchini Norway (NRK) zimeeleza kuwa mpaka sasa watu zaidi ya 50 wameripotiwa kupoteza fahamu wakiwa juu ya mlima huo na kurudishwa kwa msaada wa helkopta za serikali, chanzo kikiwa ni uoga na hali ya hewa.

Hata hivyo, Wataalamu wa miamba nchini Norway wanasema ongezeko hilo kubwa la watalii linaanza kusababisha mabadiliko ya mazingira kwenye milima hiyo hivyo kuna uwezekano wa baadae kupunguzwa idadi ya watalii wanaotembelea mwamba huo kwa siku.

Tazama picha za baadhi ya watalii wakipiga picha kwenye mwamba huo maarufu zaidi barani Ulaya.

Watalii wakiwa kwenye foleni ya kusubiri kupanda kwenye mwamba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents