Burudani

Ushauri wa RC Makonda kwa Diamond

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambaye pia ni mlezi wa WCB, amemwagia sifa msanii wa muziki Diamond Platnumz kutokana na tukio la kuzindua albamu yake ya ‘A Boy From Tandale’.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram RC Makonda ameeleza kufurahishwa na jambo hilo hivyo na kumshauri kijana huyo kuendelea kufanya kazi zake na kuacha maneno.

“Siko pekeyangu ninaejivunia kazi yako kama ambavyo haukopekeyako unaejivunia kazi yangu. Endelea kutunga nyimbo nzuri maneno tuachie wana siasa,” ameandika RC Makonda.

Siku ya jana msanii wa muziki Diamond ametengeneza historia kwa kwa kuzindua rasmi albamu yake ya ‘A Boy From Tandale’ yenye nyimbo takribani 20.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents