BurudaniDiamond PlatnumzHabari

Usiyoyajua kuhusu Jason Derule, ukubwa wake TikTok (Video)

Ukitaja jina la Jason Joel Desrouleaux alimaarufu kama @jasonderulo sio jina la kawaida kwenye kiwanda cha muziki Duniani.

Ni miongoni mwa wasanii wanaofuatiliwa sana kwa sasa mitandaoni kutokana na namna wanavyojua kuwaburudisha mashabiki zao hasa TikTok.

YouTube akaunti yake ina Subscriber milioni 33.7, ni miongoni mwa akaunti za wasanii zenye wafuatiliaji wengi sana na amewapita wasanii wengi sana YouTube.

Akaunti ina Viewers (Wafuatiliaji) zaidi ya bilioni 24 Youtube lakini pia nyimbo zake ni maarufu sana duniani na zina Viewers wengi sana.

Mfano wa nyimbo zenye Viewers wengi ni Swala aliowashirikisha Nick Minaj na Ty Dolla wenye viewers bilioni 1.7 ndani ya miaka 7 tu, lakini mwingine ni Wiggle wenye Viewers milioni 990 aliomshirikisha Snoop Dogg.

Ni wasanii wachache sana duniani waliotoa nyimbo zikafikisha Viewers bilioni moja YouTube.

Mwaka 2009 wimbo wa Watcha Say ndio uliomtambulisha zaidi kwenye kiwanda cha muziki duniani.

Jason Derule aliwahi kuwaandikia nyimbo wasanii wakubwa kama P Diddy, Sean Kingston, Cassie, Lil Wayne na wengine wengi tu.

Baadhi ya ngoma kubwa alizowahi kutoa ni kama:-

1.Swala.
2. Wiggle.
3. Talk Dirty ft. 2 Chainz.
4. Ridin’ Solo.
5. Fight for You.
6. It Girl.
7. In My Head.
8. Want to Want Me.
9. Trumpets.
10. Watcha Say.

Endapo atafanikiwa kufanya Collabo na @diamondplatnumz itasaidia sana kuupeleka mbele muziki wa Bongo Fleva na msanii husika ambaye ni Diamond Platnumz.

Ngoma ipi ni pendwa kwako kutoka kwa Jason Derule??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents