Habari

Watanzania wanazidi kuhamasika kuunga mkono filamu za ndani- Waziri Bashungwa

Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewapongeza watanzania kwa kuthamini kazi za sanaa na kuiona kuwa ni miongoni mwa sekta inayokua kwa kasi na kutoa ajira nyingi kwa vijana zinazoweza kuboresha maisha yao na kuchangia uchumi wa taifa kwa ujumla.

Mhe. Bashungwa amesema hayo alipokuwa kwenye uzinduzi wa Chama cha Tanzania Drama & Film Actors Association, (TDFAA) Ubungo Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katika uzinduzi huo Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Kitila Mkumbo ambaye ndiye Mbunge wa Jimbo la Ubungo alikuwa mgeni rasmi.

“Kupitia jukwaa hili nawashukuru sana watanzania, wanazidi kuhamasika na kuunga mkono filamu za ndani na nitaendelea kuhamasisha Balozi mbalimbali kuangalia namna ya kufanya maboresho katika filamu tunazo zitengeneza kama site location”. amesisitiza Mhe. Bashungwa

Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika siku mia moja akiwa madarakani kwa kuelekeza uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa ambapo ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo tayari Serikali imeshatenga shilingi Bilioni Moja na nusu kama kianzio.

Ameongeza kuwa, Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kurudisha Bahati nasibu ya Taifa ili makato ya asilimia 50 ya mapato yaingizwe kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Michezo.

kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha waigizaji wa filamu nchini ndugu Chiki ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaotoa kwa tasnia hiyo kupitia taasisi zilizo chini ya wizara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents