Habari

Watengeneza fedha bandia wawili wanaswa na Polisi, watuhumiwa kutapeli Mil. 20 (+video)

Watu wawili mkoani Tabora wametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za Kutengeneza Fedha Bandia na kutapeli wananchi.

Akifafanua na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema kuwa. Watuhumiwa hao wawili wamekamatwa jana Tarehe 06/02/2018 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwananchi aitwaye Daudi Jafet Mfanyabiashara kutoka Wilaya ya Kateshi Mkoa wa Manyara kuhusiana na kuibiwa fedha kiasi cha Shilingi Millioni Ishirini 20 kwa kutapeliwa fedha hizo na kupewa noti bandia.

Kamanda Nley ameeleza kuwa “Baada ya kupokea taarifa hizo misako mikali ilianza ambayo iliongozwa na taarifa zetu za kiintelijensia na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa waliotenda kosa hilo”.


Akiwataja kwa majina watuhumiwa hao ni JUMA DONALD KASHIRIKA mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa mtaa wa Rehani Kata ya Ng’ambo Tabora pia mtuhumiwa huyu ana makazi mengine mkoa wa Mbeya,
wapili ni MUSA ISAYA MWILU mwenye umri wa miaka 31 Mkazi wa mtaa wa Kwihala Kata ya Ng’ambo Tabora.

Mara baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walipekuliwa kwenye nyumba zao na kukutwa na Mabunda matano ya kutengenezea noti bandia yanayojulikana kama “KATO”, Bunda moja la Karatasi nyeupe mfano wa noti, Pesa Taslim Tsh.368,000/=,Limu moja ya karatasi, Gundi chupa moja,Mkasi,Karatasi za foil, Chupa tatu za madawa aina ya Iodine ambayo hutumika kutengenezea noti bandia pamoja na soltepu moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents