Habari

Waziri Mwakyembe awachana wabunge wanaotetea wasanii wa muziki bungeni (+video)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewatolea uvivu Wabunge wa Bunge la Jamhuri wanaotetea wasanii wa muziki nchini kufungiwa kazi zao na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kufungia kazi hizo ili kulinda maadili ya kitanzania.

Waziri Mwakyembe amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige leo Aprili 10, 2018 kwenye vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma, Swali lililohoji kwanini kamati ya maudhuni (BASATA) imekuwa na tabia ya kufungia nyimbo za wasanii ambazo tayari zimeshatoka au imeshindwa kazi?

Kwa upande mwingine, Waziri Mwakyembe ameongeza kuwa yanayotokea Tanzania yanayotokea duniani kote akitolea mfano wa nchi kama Nigeria kwa wasanii kama akina Davido na Wizkid ambao nao walishawahi kufungiwa lakini hajawahi kusikia bunge la Nigeria likitetea wasanii hao wakubwa kufungiwa nyimbo zao kama linavyofanya Bunge la Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents