Michezo

Yanga kushusha mwengine kutoka DR Congo

Mbali na winga Agee Basiala, pia Rais wa Yanga, Hersi Said kwa upande wa pili alikuwa na kazi ya kumtazama beki wa kushoto wa Lupopo, Chadrack Boka ambaye Yanga inataka aje kuchukua nafasi ya Lomalisa Mutambala.

Boka ambayeni beki mrefu anayejua kupandisha mashambulizi na kuzuia, anahesabika kuwa beki bora wa kushoto na Mazembe inamtamani kila msimu lakini inajua haiwezi kumchukua kirahisi kwa kuwa ni watani wa jadi na Lupopo na hakuna biashara inayoweza kufanyika kati ya klabu hizo mbili.

Taarifa kutoka ndani ya Lupopo ni Yanga ilishabisha hodi ndani ya klabu yao ikimtaka Boka mwisho wa msimu huu, safari ambayo uhakika bosi huyo wa Yanga ametua huko kumaliza dili hilo. Endapo kila kitu kitaenda sawa basi Yanga haitakuwa na kazi ngumu kuwapata kwani mabosi wa klabu zote ni marafiki wakubwa na tajiri wa mabingwa hao wa Tanza-nia, Ghalib Said Mohammed ‘GSM’.

Union Maniema ina urafiki mkubwa na Yanga hatua ambayo hata Simba ilipofanya jaribio la kutaka kumsomba winga Maxi Nzengeli mchakato huo ulikwama kutokana na mawasiliano ya karibu ya Yanga na tajiri wa Maniema Generali wa Jeshi la Congo Amis Kumba. Kumba maarufu kwa jina la ‘Tango Four’ ndiye mmiliki wa Maniema na kabla kigogo huyo kichaa wa soka alikuwa rais wa AS Vita Club na baada ya kung’atuka kwake timu hiyo ikapotea.

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents