Habari

Zifahamu dalili za kwamba unakabiliwa na ubaguzi kazini

Hakuna mtu anayependa mazingira magumu ya kazi. Ingawa kama unaamini hali ya ubaguzi ipo au lah, mara nyingi ni vigumu kuigundua moja kwa moja. Hivyo kuna baadhi ya tabia za kikorofi au unyanyasaji ambazo ni vigumu  kujua kama unanyanyaswa kikazi au ni jambo binafsi.

Woman sad at her desk-1512496

Je unakumbana na ubaguzi kazini? Hizi ni dalili za kujua kama unabaguliwa

Watu wengi wanaacha kazi

Kama kampuni au shirika linaendelea kwa nguvu kuajiri watu wengi inamaanisha watu wengi wanaacha kazi, hii inaashiria wafanyakazi hawapendezwi na mazingira ya kazi. Ingawa watu kuacha na kuanza kazi si kigezo pekee cha ubaguzi makazini, kwakuwa watu wengi wana kiwango cha juu cha uvumilivu hata kama mazingira ni mabaya. Kama wafanyakazi wanaacha kwa mkupuo muda si mrefu baada ya kuajiriwa hapo inamaanisha kuna tatizo kubwa. Wafanyakazi wanapaswa kufungua macho na kujua.

Maswali ya utata wakati wa Usaili

Ubaguzi wa kikazi huanza wakati wa Usaili unapoendelea. Ukiona msaili wako unauliza maswali ambayo yanaendana na mlengo fulani, labda dini, rangi, kabila au taifa kuna uwezekano mkubwa wa kutohusiana vizuri na wewe hata akikuajiri. Mashirika na makampuni mengi kisela yanaruhusu watu wa aina tofauti tofauti na imani tofauti ingawa sio mameneja wote wanaokubalilana na hali hiyo. Hivyo inamaanisha kwamba watu wa mlengo mmoja na bosi au mwajiri huajiriwa kirahisi sana. Igawa udhalilishaji(kijinsia na kihisia) na maonezi hutokea wakati umeanza kazi.

Utaratibu mbaya wa kupanga kazi kwa wafanyakazi

Wafanyakazi wanaotengwa hupewa kazi ndogo au chache zisizo na tija  ama wakati mwingine hupewa kazi ngumu zisizoisha kirahisi. Mkakati huu unakuwa kuwatengenezea nafasi wale ambao ni wa mlengo wake ambao mara nyingi hawana uwezo wa kufanya kazi ila hupandishwa vyeo na kuongezewa mishahara na wakati mwingine kutengeneza mazingira ya kumachisha kazi mfanyakazi anayetengwa.

Namna ya mazungumzo yanavyofanyika na mabosi

Sehemu nyingine ya kutengwa kazini huhusisha namna kiongozi au bosi anavyoongea na mtu asiyempenda au kutomtaka. Kama mara nyingi unafokewa na kusemeshwa kwa ukali bila sababu tambua ya kuwa kuna kitu kinaendelea. Wakati mwingine utani usiokuwa wa manufaa kwako. Na mambo haya hulenga hasa dini, kabila, & umri.

Kama unahisi mambo si ya kawaida kazini kwako, jaribu kuomba ushauri na vilevile mwanasheria au taasisi inayohusika na matatizo kazini kwa msaada zaidi. Usijaribu kushughulikia tatizo peke yako.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents