Habari

Afande Sele amjia juu Mhe. Sugu ‘ulimtukana Rais jukwaani, matendo yako ndio yamemuua mama yako’

Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Tanzania, Afande Sele amesema kuwa kwa upande wa vyama vya upinzani ni Professor Jay pekee ndiye Mbunge anayeonekana kufanya kazi kwa bidii huku akimtolewa mfano Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuwa anaendekeza siasa chafu za matusi jukwaani.

Sugu na Afande Sele

Afande Sele amefunguka hayo kupitia mahojiano yake na Bongo5, ambapo amedai kuwa kauli ya Sugu kuwa mama yake amefariki kutokana na tukio la yeye kufungwa jela hilo ni kosa lake kwani alimtukana mkuu wa nchi, Rais Magufuli jukwaani jambo ambalo ni kosa kisheria. Sikiliza mahojiano yake hapa chini

Mhe. Sugu wiki iliyopita Agosti 28, 2018 wakati wa kuuaga mwili wa marehemu mama yake jijini Dar es salaam, alisikika akisema kuwa mama yake alizidiwa zaidi na presha baada ya tukio la yeye kufungwa jela kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli jukwaani, ambapo hadi mama yake anakufa alikuwa anaamini kuwa mtoto wake alifungwa kwa kuonewa jambo ambalo lilipelekea homa yake ipande.

 

Related Articles

74 Comments

  1. Jamani wa tz,uyu seleh sio hata bifu la vyama inakua ni wivu wa maisha sasa,tulia na maneno yako ya fitna aho malegends wenzako wanaweza kukusaidia seleh ,fitna sio nzuri ,miaka nenda miaka rudi aujapata mafanikio nawakati we we ni mchapaka Nazi ,unajua kwanini aufanikiwi?
    Jibu=fitna na roho ya unafiki ,,

  2. Nyota yako Afande selle ilikuwa mbovu toka zamani enzi za usanii wako na aliyekuwa anakubeba ni sugu kwaiyo mpka sasa ndio umezidi kupoteana kabisa levo yako bado ndogo sana usijilinganishe na sugu brother sio levo yako uyo jamaa

  3. Wanao mtus afande warudie kusoma naona hamkumulewa nyinyi nihuo uchungu wa sugu nn kama ni mama kasha kufa sasa nn tena uchungu wamwana aujuaye mzaz kwasasa ukija na siasa ya kashfa utapopea siasa sio maneno machafu siasa nihekima na utulivu bas

  4. Kutokana nakauli ilokuepo kwamba mama kauliwa na uchungu wa mwanae kupata matezo kwanihaya nayo yalizungumzwa wakat mama kafufuka ww ndohujilew wafikir hata sugu akipata urais atakujua apigania njaa yake yule na familia yake kwatarifa yako usiumizwe kichwa na vitu vya hovyo kaa utulie chamΓ‘ ni ccm milele daima

  5. Huyu afande atakua mchawi sio bure na roho mbaya ndo inamtesa zaidi hayo ni maumiv tu ya sugu na profesa kuwa wabunge kiroho kinakusonona uchaw sio lazma ukutwe juu ya paa unawanga hata kauli zako pia zitakutambilish km ni mchaw na una roho ngum loooh sura imemkauka km kanywa sumu

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents